Rais wa Namibia ameeleza matarajio yake ya kustawishwa uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza hii leo huko Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Iran Ali Akbar Salehi, Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia amepongeza
uchaguzi wa rais nchini Iran na kueleza kuwa, matokeo na namna duru ya
11 ya uchaguzi wa rais wa Iran ulivyoendeshwa vinaonyesha jinsi wananchi
wa Iran wanavyounga mkono demokrasia. Rais wa Namibia meashiria
uhusiano wa kihistoria wa wananchi wa Namibia kupitia ofisi ya Swapo
hapa mjini Tehran na kueleza kuwa Iran ilidhihirisha urafiki wake wa
kweli na Namibia kwa kufungua ofisi ya harakati ya Swapo kabla ya uhuru
wa nchi hiyo na kuendelezwa mahusiano kati ya nchi mbili hizi hata baada
ya Namibia kupata uhuru.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria
irada ya viongozi wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya
kutaka kuwa na uhusiano mzuri na Namibia na kueleza kuwa Iran imepata
mafanikio na maendeleo makubwa katika nyuga mbalimbali katika kipindi
cha miaka 34 iliyopita na sasa iko tayari kutoa uzoefu na utaalamu wake
huo kwa nchi nyingine rafiki ikiwemo Namibia.
No comments:
Post a Comment