Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge Dakta Ali
Larijani amesema kuwa mashirika ya ujasusi ya nchi za nje yanayaunga
mkono makundi ya wanamgambo wanaowakufurisha Waislamu wengine katika
nchi za Kiislamu ikiwemo Misri. Larijani amesema mkono wa mashirika hayo
ya ujasusi umeshuhudiwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Iraq,
Afghanistan na Misri. Ameongeza kuwa makundi hayo yanayowakufurisha
Waislamu wengine daima yamekuwa balaa kubwa kwa Uislamu.
Spika wa
Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema makundi hayo yanadai kuwa
yanafanya Jihad na akahoji ni Jihadi gani hiyo inayoruhusu kuua
Waislamu. Ali Larijani amesema baadhi ya serikali za Magharibi
zimekutana na makundi hayo yenye kufurutu ada huko Iraq na kuyaahidi
kuyaunga mkono katika mapambano yake dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya
Shia na Jamhuri ya Kiislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment