Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Saeed Jalili
amesema kuwa, Marekani si nchi ya kuaminika na haifai kufanya ushirika
nayo. Jalili ameyasema hayo leo hapa mjini Tehran alipokutana na kufanya
mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan, Ershad
Ahmadi kuhusu uhusiano wa pande mbili. Jalili ameongeza kuwa, 'sera za
kigeni za Marekani katika eneo hili ni ishara ya wazi kuwa Washington
inapinga umoja, uthabiti na ustawi wa nchi za Kiislamu.' Amesema
imeibainikia jamii ya kimatiafa hasa watu wa eneo kutoka Afghanistan
hadi Misri kuwa, madai ya Marekani ya kupambana na ugaidi na kuunga
mkono demokrasia ni uongo mtupu.'
Afisa huyo wa Iran amesema kuwa,
'kuunga mkono ugaidi na kupinga demokrasia ndio msingi wa sera za
Marekani katika eneo hili.'
Jalili pia amesema, kuna haja ya kuimarisha uhusiano wa Iran na
Afghanistan. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Afghanistan ameipongeza serikali ya Iran kwa kuendelea kuwasaidia watu
wa Afghanistan katika kipindi chote cha masaibu nchini humo. Ameelezea
matumaini yake kuwa uhusiano wa Tehran na Kabul utaimarika zaidi baada
ya vikosi vya nchi za Magharibi kuondoka kabisa katika eneo hili.
Ikumbukwe kuwa Marekani na waitifaki wake waliivamia Afghanistan mwaka
2001 katika kile kilichodaiwa kuwa eti ni vita dhidi ya ugaidi. Hata
hivyo hadi leo Afghanistan bado imesakamwa na jinamizi la ugaidi.
No comments:
Post a Comment