Serikali na wananchi wa Bolovia wamelaani hatua ya Ufaransa na Ureno ya
kukataa ndege ya rais wao, Evo Morales kutumia anga yao na kusema jambo
hilo lilikuwa na lengo la kumvunjia heshima na kuhatarisha maisha yake.
Rais Morales alikuwa akirudi nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa
kimataifa wa nishati nchini Russia. Ndege yake ililazimika kutua kwa
dharura mjini Vienna, Ausria baada ya Ufaransa na Ureno kukataa ndege
isipae katika anga yao.
Nchi hizo zilidai kwamba uamuzi huo
ulisababishwa na hitilafu za kiufundi lakini duru zimefichua kwamba
Paris na Lisbon zilishuku huenda Rais Morales alikuwa ameandamana na
afisa wa zamani wa CIA ya Marekani anayesakwa, Bw. Edward Snowden.
Jasusi huyo wa zamani wa Marekani anasakwa na nchi yake baada ya
kufichua kwamba CIA na mashirika mengine ya kijasusi ya Washington
yamekuwa yakifanya ujasusi dhidi ya watu kote duniani wakiwemo
wanadiplomasia kwa kusikiliza kwa siri mazungumzo yao ya simu na kudukua
baruapepe zao. Jambo hilo limezusha hasira kote duniani huku Umoja wa
Ulaya ukitishia kuvunja mikataba ya kibiashara na Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment