Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametishia kujiondoa nchi yake kwenye
uanachama wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC. Taarifa
zinasema kuwa, tishio hilo la serikali ya Zimbabwe limetolewa baada ya
kutolewa msisitizo wa jumuiya hiyo wa kufanyika marekebisho ya
demokrasia kabla ya kufanyika uchaguzi ujao wa rais na bunge nchini
humo. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wafuasi wa
chama chake cha Zanu PF, Rais Mugabe amesema kuwa, maamuzi ya SADC siyo
ya kimantiki, na kusisitiza kwamba Zimbabwe inaweza kujiondoa kwenye
jumuiya hiyo.
Awali Rais Mugabe alitangaza kuwa, uchaguzi ujao
ungelifanyika tarehe 31 Julai, lakini wapatanishi kutoka SADC
walishinikiza uchaguzi huo usogezwe mbele kwa muda wa wiki mbili, ili
yaweze kufanyika marekebisho ya kidemokrasia nchini humo. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, Godfrey Chidyausiku Jaji Mkuu wa Zimbabwe amesema
kuwa, Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo haina mamlaka ya kubadilisha
tarehe ya uchaguzi wa rais iliyotangazwa hapo awali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment