Alexei Navalny kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini Russia ambaye
alitiwa mbaroni na jeshi la polisi kwenye maandamano hapo jana, huenda
akatumikia kifungo cha miaka sita jela. Waendesha mashtaka nchini Russia
wameitaka Mahakama ya Kirov nchini humo kumfunga Navalny kwa tuhuma za
kufanya ubadhirifu mkubwa wa mali nchini humo. Iwapo hukumu hiyo
itatolewa, itamfanya kiongozihuyo wa upinzani ashindwe kushiriki kwenye
uchaguzi wa raia utakaofanyika mwaka 2018 nchini humo.
Waendesha
Mashtaka hao wa Russia wameitaka mahakama hiyo kumpiga faini ya dola
elfu thelathini. Navalny anatuhumiwa kwa kulitia hasara dola laki tano
kwenye bajeti iliyotengwa katika jimbo la Kirov wakati alipokuwa
akihudumu kama Gavana wa jimbo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment