Jeshi la Mali limeituhumu harakati ya Azawad MNLA kwa kukiuka makubaliano ya amani yaliyofikiwa nchini Burkina Faso.
Kanali Diarran Kone kutoka Jeshi la Mali amesema kuwa, harakati ya
Azawad tangu Jumamosi iliyopita imekuwa ikiwakusanya wanawake na watoto
wa eneo la Kidal, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuwashambulia
wanajeshi wa Mali na askari wa kulinda amani kutoka nchi za Kiafrika.
Amesema kuwa, harakati hiyo iliwashawishi wananchi wa eneo la Kidal
kufanya maandamano wakati yalipoingia majeshi ya kulinda amani ya
Kiafrika MINUSMA na kujeruhi wanajeshi kadhaa. Wanajeshi 150 wa Mali
Ijumaa iliyopita waliingia kwenye mji wa Kidal, baada ya kufikiwa
makubaliano ya amani ya pande hizo mbili Juni 18 nchini Burkina Faso.
No comments:
Post a Comment