Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 9, 2013

Iran, IAEA kukutana mwezi ujao wa Agosti

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA unatarajiwa kufanya duru mpya ya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwezi ujao wa Agosti.
Mazungumzo hayo yatajadili kwa kina kadhia ya Nyuklia ya Iran ambapo mwanadiplomasia mmoja wa wakala huo amesema kwamba, kuna matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kiwango fulani.
Mwanadiplomasia huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amedai kuwa, kwa kuzingatia kwamba mazungumzo hayo yatakuwa ya kwanza tangu baada ya uchaguzi wa rais wa mwezi Juni, huenda serikali mpya ya Rais mteule Hassan Rohani ikawa na misimamo ya wastani kwenye mazungumzo ikilinganishwa na serikali inayoondoka ya Rais Mahmoud Ahmadinejad.
Dkt. Rohani anafahamika kwa misimamo yake ya wastani na wengi katika ulimwengu wa Magharibi wamempa jina la 'Sheikh Mwanadiplomasia.'

No comments: