Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamefunguliwa leo
mjini Tehran na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maonyesho hayo ya kimataifa yameanza alasiri ya leo katika uwanja mkubwa wa swala wa Imam Khomeoni.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka huu yana vitengo 40 vikiwemo
vya majarida ya Qur'ani, vyuo vikuu vya kidini na visivyo vya kidini,
tarjumi ya Qur'ani Tukufu, Qur'ani, Vijana na watoto, mwenendo wa maisha
ya Kiqur'ani, Qur'ani na dini mbalimbali, Qur'ani na sayansi, Qur'ani
na umoja wa Kiislamu na kadhalika.
Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yataendelea kwa kipindi cha wiki moja.
No comments:
Post a Comment