Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia hali ya
sasa ya Misri na kitendo cha jeshi la nchi hiyo cha kumuondoa madarakani
rais aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Mursi na kusema, Misri ni
kituo cha mwamko wa Kiislamu na kwamba wale waliopewa dhima ya kuunda
serikali baada ya mapinduzi ya wananchi Waislamu walijitayarishia uwanja
wa kupinduliwa na kuondolewa madarakani.
Ayatullah Ahmad Khatami amewataka wananchi wa Misri kulinda mwamko
wao wa Kiislamu na wasiruhusu tena nchi hiyo kuwa mwandani wa utawala wa
Kizayuni wa Israel kama ilivyokuwa serikali iliyoondolewa madarakani ya
Hosni Mubarak.
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, wale waliounda
serikali iliyopita ya Misri awali walitoa nara za kupambana na utawala
ghasibu wa Israel lakini baada ya kushika madaraka walirefusha mkataba
wa Camp David na kumwita rais wa utawala ghasibu wa Israel Shimon Perez
kuwa ni ndugu yao!
Ayatullah Ahmad Khatami pia ameashiria tukio la kusikitisha la kuuawa
Sheikh Hassan Shehata aliyekuwa miongoni mwa maulama wa madhehebu ya
Kiislamu ya Shia nchini Misri na kusema, uwahabi ambao wafuasi wake ndio
waliomuua kinyama msomi huyo, ulibuniwa na Waingereza na umeendelea
kuwepo kwa kutumia sera za mauaji. Amewataka maulamaa wa Kisuni
kupambana na wasababishaji wa mauaji hayo na kutangaza waziwazi kwamba
Uwahabi hauna uhusiano wowote na dini ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment