Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 6, 2013

Hali ya kiafya ya Mandela yazidi kutatanisha

Serikali ya Afrika Kusini leo Ijumaa imekanusha madai kwamba hali ya mzee Nelson Mandela ni mbaya mno na kwamba madaktari wameshauri aondolewe kwenye mashine ya kupumulia.
Taarifa ya serikali imesema kuwa, shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini bado yuko katika hali mahututi lakini anaonyesha dalili nzuri za kupata nafuu.
Hata hivyo barua iliyowasilishwa kortini siku ya Jumatano na baadhi ya watu wa familia ya Mandela inaonyesha kwamba kiongozi huyo wa zamani kwa mtazamo wa kitiba tayari amefariki dunia, lakini anasaidiwa na mashine. Barua hiyo pia imesema kwamba madaktari wameishauri familia ya Madiba izime mashine hiyo ili kupunguza gharama na kutoa fursa ya kuandaliwa maziko ya heshima kwa mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel.
Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo kwamba, familia ya Mandela inafaa kuchukua maamuzi magumu lakini haipaswi kushinikizwa na mtu yeyote.

No comments: