Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, July 5, 2013

Ijumaa, Julai 05, 2013

Leo ni Ijumaa tarehe 26 Shaaban 1434 Hijria, inayosadifiana na tarehe 5 Julai 2013.
Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita wananchi wa Algeria walipata uhuru baada ya mapambano ya miaka mingi dhidi ya wakoloni wa Kifaransa na baada ya kuuawa shahidi Waalgeria milioni moja. Wakoloni wa Kifaransa waliivamia Algeria mwaka 1830 na kukabiliana na mapambano makali ya Waalgeria wakiongozwa na Amir Abdulqadir al Jazairi.
Hata hivyo jemedari huyo wa uhuru wa Algeria alikamatwa na Wafaransa baada ya mapambano ya miaka 17 na sehemu kubwa ya nchi hiyo ikatwaliwa na wakoloni hao. Mwanzoni mwa karne ya 20 ardhi yote ya Algeria ilikaliwa kwa mabavu na Wafaransa. Harakati ya uhuru wa Algeria ilipamba moto tena baada ya Vita vya Pili vya Dunia na hatimaye ilimlazimisha Jenerali Charles de Gaulle wa Ufaransa kutia saini mkataba wa Evian ulioipa uhuru kamili Algeria.
Tarehe 5 Julai miaka 36 iliyopita Jenerali Muhammad Zia-ul-Haq alitumia hali ya mgogoro iliyokuwa ikitawala Pakistan na kufanya mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya Zulfiqar Ali Bhutto. Muhammad Zia-ul-Haq alitwaa madaraka yote ya waziri mkuu na rais wa Jamhuri ya Pakistan na mbali na kuwanyonga Zulfiqar Bhutto na wapinzani wake wengine, alivunja mabunge ya nchi hiyo na kusimamisha shughuli zote za vyama vya siasa nchini Pakistan.
Na miaka 31 iliyopita katika siku inayosadifiana na ya leo wanadiplomasia watatu na mwandishi habari mmoja wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitekwa nyara na wapiganaji wa chama cha Falanja cha Lebanon kaskazini mwa Beirut. Wanadiplomasia hao na mwandishi wa habari wa Iran walitekwa nyara wakati walipokuwa wakielekea kazini katika ubalozi wa Iran huko Beirut. Wakati tukio hilo lilipojiri jeshi la utawala wa Kizayuni lilikuwa limeishambulia Lebanon na chama cha Falanja kilikuwa na ushirikiano wa karibu na utawala ghasibu wa Israel. Ushahidi na nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa raia hao wa Iran wanashikiliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments: