Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, July 5, 2013

Dola bilioni moja zahitajika kwa ajili ya eneo la Sahel

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba unahitaji zaidi ya dola bilioni moja kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula ya watu wanaokabiliwa na njaa katika eneo la Sahel barani Afrika. Robert Piper afisa wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA amesema kuwa, vita vya mwaka huu nchini Mali ambako askari wa Ufaransa waliongoza mapambano dhidi ya waasi vimesababisha ukosefu mkubwa wa chakula kwenye eneo hilo.
Ameongeza kuwa, wafadhili wametoa dola milioni 607 tu na inakadiriwa kuwa, zinahitajika zaidi ya dola bilioni 1.72 ili kusaidia watu wa eneo la Sahel wasikose chakula na kupata utapiamlo. Afisa huyo wa OCHA ametahadharisha kuwa, mgogoro wa Syria umewasahaulisha wafadhili  hali mbaya ya eneo hilo la Afrika. 

No comments: