Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 6, 2013

AU yasimamisha uanachama wa Misri

Umoja wa Afrika (AU) leo Ijumaa umesimamisha uanachama wa Misri kufuatia kile ulichokitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali halali iliyochaguliwa kidemokrasia na wananchi.
Taarifa ya Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika imesema kwamba, hatua ya kusimamisha uanachama wa Misri inakwenda sanjari na katiba ya AU ambayo inapinga hatua yoyote ya kuchukua madaraka ya nchi kwa njia zisizo za kidemokrasia.

Hata hivyo, balozi wa Misri katika Umoja wa Afrika, Muhammad Idris amesema yaliyofanyika Misri ni utekelezwaji wa matakwa ya wananchi na wala sio mapinduzi. Ameongeza kuwa, Wamisri wamezungumza kwa kauli moja na kwamba hatua ya jeshi ilikuwa ni kuepusha nchi kutumbukia kwenye machafuko.
Kwa sasa, Misri imejiunga na nchi kama vile  Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar ambazo zimevuliwa uanachama na AU kutokana na serikali zilizoko kuingia madarakani kinyume na njia za kidemokrasia.

No comments: