Jeshi la Misri limemuuzulu Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo na
kusimamisha katiba, hatua ambayo imechukuliwa ili kututua mgogoro wa
kisiasa wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa maafisa wa ngazi za juu wa Harakati
ya Ikhwanul Muslimin ya Misri, Mursi anashikiliwa katika jengo la Wizara
ya Ulinzi pamoja na wasaidizi wake wa ngazi za juu.
Jeshi la Misri limetoa taarifa ya kusimamishwa katiba na kuteuliwa
aliyekuwa mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba Adly Mansour kuwa kiongozi wa
mpito wa Misri. Mansour anatarajiwa kuapishwa hii leo.
Wakati huo huo watu wasiopungua 14 wameuawa na wengine kadhaa
kujeruhiwa nchini Misri katika machafuko yaliyotokea kati ya wanaomuunga
mkono Musri na wanaopinga baada ya jeshi kumuondoa madarakani kiongozi
huyo.
Katika upande mwingine kiongozi wa upinzani Mohamed al Baradei
amesema, ramani ya njia iliyotangazwa na jeshi la Misri inakidhi matakwa
ya wananchi ya kufanyika uchaguzi wa mapema.
No comments:
Post a Comment