Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan amemtimua kazi Waziri wa Ulinzi
wa nchi hiyo Mohammed al Barghathi baada ya kutokea mapigano makali
mjini Tipoli baina ya makundi mawili yenye silaha ambayo yamesababisha
vifo vya watu watano na kujeruhi makumi ya wengine.
Ali Zeidan amesema baada ya yaliyojiri jana imeamuliwa kwamba Waziri
wa Ulinzi ataachichwa kazi. Tutatanganza waziri mpya wa ulinzi hivi
karibuni, amesisitiza Waziri Mkuu wa Libya.
Uamuzi huo wa kumfuta kazi Waziri wa Ulinzi wa Libya umechukuliwa
huku nchi hiyo ikusumbuliwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi
ya wanamgambo wanaobeba silaha.
Jumatano iliyopita watu wengine 5 waliuawa na makumi ya wengine
kujeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea baina ya makundi hasimu
kwenye wilaya ya Salahuddin. Mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya wa
Benghazi pia umekumbwa na machafuko makubwa ambapo vituo kadhaa vya
polisi vimelipuliwa kwa mabomu.
No comments:
Post a Comment