Jumuiya zisizokuwa za serikali zimetangaza kuwa Jamhuri ya Afrika
ya Kati inasumbuliwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu tangu baada ya
harakati ya waasi wa Seleka kutwaa madaraka ya nchi mjini Bangui mwezi
Machi mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na jumuiya hizo imesema wakazi wote milioni 4.6
wa Jamhuri ya Afrika ya kati wanasumbuliwa na athari mbaya za mgogoro wa
kibinadamu uliofuatia mapindizu ya Seleka na machafuko ya kisiasa.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unasema Jamhuri ya
Afrika ya Kati inahitaji msaada wa yuro milioni 97 na kwamba ni asilimia
43 ya msaada huo iliyokusanywa hadi hivi sasa.
Taarifa hiyo imeashiria matatizo makubwa yanayowakabili watu wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati kama ukosefu wa huduma za afya na chakula,
wizi, mauaji ya holela na kubakwa wanawake hususan watoto wadogo.
Imesisitiza kuwa mgogoro wa sasa katika Jamhuri ya Afika ya Kati ndio
mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
No comments:
Post a Comment