Watu wasiopungua 48 wameuawa na nyumba nyingi kuteketezwa moto kufuatia mapigano ya kikabila katika eneo la kati mwa Nigeria.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria katika jimbo la kati la Plateau
Kapteni Salisu Mustapha amesema kati ya waliopoteza maisha ni wakaazi
28 wa kijiji cha Langtang na wavamizi 20 ambao waliuawa na wanajeshi
walioitwa kutuliza hali ya mambo.
Viongozi wa kijamii wanasema machafuko
hayo ya Alkhamisi yaliibuka kufuatia msururu wa wizi wa mifugo katika
jimbo hilo. Wanakijiji wengi wanaripotiwa kukimbia makaazi yao kwa
kuhofia machafuko zaidi baina ya makabila hasimu ya Fulani na Tarok.
Maelfu ya Wanigeria wamepoteza maisha katika mapigano ya kikabila katika
eneo la kati mwa nchi hiyo. Aidha eneo la kaskazini mwa Nigeria pia
limeshuhudia machafuko katika miaka ya hivi karibuni ambapo maelfu ya
watu pia wamepoteza maisha kufuatia uasi wa kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment