Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaja bara la Afrika
kuwa ni bara lenye kupiga hatua kimaendeleo. Akizungumza na vyombo vya
habari mjini New York, Ban Ki moon amesema kuwa nchi nyingi za Kiafrika
zimefanikiwa katika kuleta amani, kupunguza kiwango cha umasikini,
kuongeza kipato cha wananchi na kupiga hatua kubwa katika mapambano
dhidi ya maradhi hatari, kama vile malaria na ukimwi.
Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, Waafrika wameweka azma ya kuimarisha
demokrasia, na hali kadhalika kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki
za binadamu na ufisadi. Hata hivyo, Ban Ki moon amesisitiza kuwa, nchi
za Kiafrika bado zinakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo amewataka
viongozi na Waafrika kwa ujumla kupiga hatua zaidi ili kukabiliana na
changamoto hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment