Ijumaa hii kumeshuhudiwa maandamano makubwa katika mji
mkuu wa Misri, Cairo baina ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammad
Mursi.
Wafuasi wa Mursi walikusanyika nje ya msikiti mkubwa wa
eneo la Nasr huku wapinzani wakikutana katika Medani ya Tahrir. Wakiwa
hapo wakijaribu bila mafanikio kuandamana hadi katika Ikulu ya Rais.
Baadhi ya duru za habari zinaarifu kuwa Rais Mohammad Mursi
ameukimbia mji wa Cairo na kuenda eneo lisilojulikana. Aidha imearifiwa
kubwa Ubalozi wa Marekani mjini Cairo utafungwa kwa siku kadhaa kwa
kuhofia hujuma ya waandamanaji.
Wapinzani nchini Misri wameitisha maandamano makubwa kote
nchini humo Juni 30 ambapo wanataka kumlazimisha Rais Mursi ajiuzulu.
Wanamlaumu kiongozi huyo kuwa amekengeuka mkondo wa mapinduzi
yaliyomtimua madarakani dikteta Hosni Mubarak. Uamuzi wa Mursi wa kukata
uhusiano na Syria na kuwaunga mkono magaidi nchini humo pia ni jambo
ambalo limewakasirisha wananchi wa Misri.
No comments:
Post a Comment