Watu walioomba hifadhi ya kisiasa katika mji wa Munich nchini Ujerumani
na kufanya mgomo wa kula hadi yatakapotekelezwa matakwa yao, wamegoma
kulishwa vyakula vya majimaji na wametishia kujiua. Watu hao wanaofikia
idadi yao 50 kutoka nchi za Nigeria, Ethiopia, Pakistan na nchi nyingine
wamesisitiza kuwa hawatalegeza kamba hadi litakapotekelezwa takwa lao
la kupewa hifadhi ya kisiasa nchini humo.
Timu ya madaktari imeeleza
kuwa, kitendo cha wanasiasa hao kukataa kula na kunywa kitahatarisha
zaidi maisha yao. Duru za hospitali zinaeleza kuwa, wafanya mgomo 19
wamefikishwa hospitali, akiwemo mama mmoja mwenye watoto wawili baada ya
hali zao kuwa mbaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment