Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin nchini Misri imetangaza kuwa haitatoa
mwanya wa kupinduliwa utawala wa Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo.
Mohammad al Beltagui mbunge na kiongozi mwandamizi wa harakati ya
Ikhwanuul Muslimiin amewahutubia maelfu ya wafuasi wa Rais Morsi mjini
Cairo na kusisitiza kuwa, harakati hiyo kamwe haitatoa fursa kwa
wapinzani kufanya mapinduzi yatakayopelekea kumuondoa madarakani Rais
Morsi.
Al Beltagui amesisitiza kuwa, serikali ya Morsi haiwezi
kufananishwa na utawala wa Hosni Mubarak dikteta aliyeondolewa
madarakani nchini humo, na kuongeza kuwa, wapinzani hawana uwezo wa
kutekeleza mapinduzi mengine nchini humo. Duru za habari zinasema kuwa,
Rais Morsi pamoja na familia yake ameondoka kwenye Ikulu ya nchi hiyo na
kuelekea mahala pasipojulikana, kukwepa maandamano makubwa
yatakayofanywa na wapinzani hapo kesho Jumapili nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment