Mamia ya waandishi habari wa nchi za kigeni tayari wawo hapa
nchini kwa ajili ya kuakisi uchaguzi wa rais wa Iran unaofanyika leo
Juni 14. Alireza Shirvani Mkuu wa ofisi ya Maripota wa Kigeni ya Wizara
ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, karibu
waandishi habari 430 wanaowakilisha mashirika tofauti ya habari yapatayo
190 kutoka nchi 40 duniani wapo hapa nchini kwa ajili ya kuakisi zoezi
la uchaguzi wa rais.
Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iran ametangaza
kuwa vituo 60 elfu vya kupigia kura nchi nzima viko tayari kwa ajili ya
zoezi la uchaguzi wa rais wa Iran na Mabaraza ya Miji na Vijiji
unaofanyika leo.
Mustapha Muhammad–Najjar ameeleza kuwa, kura zitaanza
kupigwa saa mbili asubuhi leo Ijumaa na zoezi hilo litaendelea kwa masaa
10 hadi saa 12 jioni na kwamba iwapo itahitajika muda utaongezwa kwa
mujibu wa sheria. Muhammad-Najjar aidha amesisitiza kuwa, kura zitaanza
kuhesabiwa baada tu ya upigaji kura kumalizika na kwamba katika duru
hii ya uchaguzi jitihada zitafanywa ili matokeo yatangazwe haraka
iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment