Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 14, 2013

Uhuru: Nchi za EAC zishajiishe uwekezaji wa ndani

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka sera madhubuti zitakazoshajiisha utegemezi wa ndani katika masuala mbalimbali hususan uwekezaji. Rais Kenyatta amesema wawekezaji wa kigeni wameanza kupungua barani Afrika kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi zao na kwa mantiki hiyo pana haja ya kuboresha mazingira kwa ajili ya kuinua uwekezaji wa ndani.
Kauli ya rais wa Kenya imetolewa huku maoni na hisia mbalimbali zikiendelea kujitokeza siku moja baada ya nchi za Afrika Mashariki kusoma kwa pamoja bajeti zao za mwaka 2013/2014. Nukta inayozikutanisha pamoja bajeti hizo ni suala la kuongezwa kodi kwa bidhaa za anasa kama vile pombe, sigara, simu za mkononi na magari.

No comments: