Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mohamed Kamel Amr amesema kuwa nchi
yake imekubaliana kuendeleza mazungumzo zaidi na Ethiopia ili kujadili
na kutatua mgogoro wa maji ya Mto Nile kwa njia za kidiplomasia. Kamel
Amr amesema mazungumzo hayo yatafanyika katika ngazi za kisiasa na
kitaalamu ili kutathmini athari zitakazojitokeza iwapo Ethiopia itaamua
kuendelea na ujenzi wa bwala la Renaissance.
Msimamo wa Misri unafuatia
mkutano wa hapo jana kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia na
Misri mjini Addis Ababa. Mgogoro huo umepelekea kuzuka vita vya maneno
kati ya Cairo na Addis Ababa ambapo Misri huko nyuma ilitishia kutumia
nguvu za kijeshi kusimamisha ujenzi wa bwawa hilo. Cairo inadai maji ya
Mto Nile ni uti wa mgongo wa uchumi wake na kwamba juhudi zozote za
kuipunguzia maji ya mto huo ni sawa na kukata mshipa wake wa pumzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment