Zaidi ya viongozi 10 wa nchi na serikali kutoka nchi mbalimbali za dunia
wanakutana mjini Dar es Salaam Tanzania kujadili ushirikiano wa
kibiashara. Mkutano huo unaojulikana kama Smart Partnership
International Dialogue 2013 utafunguliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete
alasiri ya leo na miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na jinsi
ya kutumia teknolojia ya kisasa kuinua uchumi wa nchi zinazoshiriki.
Miongoni mwa marais wanaohudhuria ni pamoja na Uhuru Kenyatta (Kenya),
Yoweri Museveni (Uganda), Mahinda Rajapaksa (Sri Lanka), Ikililou
Dhoinine (Comoro), Mfalme Mswati II (Swaziland).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment