Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Rwanda imetangaza kuwa, takriban
watu milioni 6 wanatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi wa bunge
uliopangwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Watu milioni 4.8 ndio walioshiriki kwenye uchaguzi wa bunge wa mwaka
2008. Mwenyekiti wa tume hiyo, Prof. Kalisa Mbanda amesema matayarisho
yanakaribia kukamilika na kwamba uchaguzi huo utagharimu Faranga bilioni
5.
Amesema kutokana na maafisa wake kupata uzowefu wa kutosha, gharama
za zoezi hilo zimepungua ikilinganishwa na mwaka 2008 ambapo fedha
zilizotumika zilikuwa Faranga bilioni 9.
Tayari baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamerudi Rwanda
kutoka nchi za nje kwa ajili ya kuandaa vyama vyao kwa uchaguzi huo.
Rais Paul Kagame majuma kadhaa yaliyopita alitoa onyo kali kwa wanasiasa
waliorudi nyumbani akisema wale watakaojaribu kutumia mwanya wa kampeni
kuwagawa wananchi watakabiliwa na mkono mrefu wa sheria.
No comments:
Post a Comment