Maelfu ya watu wenye hasira wamefanya maandamano makubwa katika
maeneo mbalimbali ya Misri wakimtaka Rais Muhammad Morsi ajiuzulu.
Maelfu ya waandamanaji leo jioni wamekusanyika katika Medani ya
Tahrir mjini Cairo kushinikiza Rais Morsi aondoke madarakani na
kufanyike uchaguzi wa kabla ya wakati wake.
Huko mjini Alexandria, mji wa pili kwa ukubwa nchini Misri nako,
maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali ya Cairo wamekusanyika kwenye
medani kubwa za mji hiyo.
Mjini Port Said pia maelfu ya wapinzani wa serikali ya Misri wamefanya maandamano kutaka Rais Morsi ajiuzulu.
Maandamano hayo yameitishwa na wapinzani katika maadhimisho ya mwaka
mmoja wa tangu Muhammad Morsi achaguliwe kuwa rais wa nchi hiyo ya
kaskazini mwa Afrika.
Waandamanaji hao wanadai kuwa, Morsi ameshindwa kutekeleza malengo ya
mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani dikteta Hosni Mubarak.
Katika upande mwingine, maelfu ya wafuasi wa Morsi nao wameandamana
wakisema kuwa, rais huyo amechaguliwa na wananchi na kuwataka wapinzani
waheshimu demokrasia.
No comments:
Post a Comment