Vyama na makundi ya kisiasa yanayoipinga serikali ya Algeria vimetaka
kufanyika uchaguzi wa kabla ya wakati kwa mujibu wa katiba kutokana na
kuugua rais wa nchi hiyo. Vyama vingi vya upinzania vinataka kufanyika
uchaguzi wa kabla ya wakati huko Algeria na kutangazwa rais mpya
atayechukua majukumu ya kuiongoza nchi. Jahid Yonus Katibu Mkuu wa
Harakati ya Kitaifa ya Marekebisho ya Algeria amesema kuwa vyama na
makundi ya kisiasa nchini humo yanapasa kufikia makubaliano na kumchagua
mgombea mmoja atakayeshiriki katika uchaguzi ujao wa rais.
Katibu Mkuu
wa Harakati ya Kitaifa ya Marekebisho ya Algeria amekosoa utendaji wa
kisiasa wa baadhi ya viongozi wa serikali na kutahadharisha kuwa, mfumo
wa uongozi wa Algeria unaelekea upande wa mfumo wa kifalme. Jahid Yunisi
ameongeza kuwa, viongozi wa serikali ya Algeria wanadhibiti vyombo vya
habari ili kupotosha fikra za walio wengi nchini humo. Rais Abdulaziz
Butafliqa wa Algeria hivi sasa amelazwa hospitalini nchini Ufaransa
baada kupatwa na kiharusi siku kadhaa zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment