Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali
Khamenei leo asubuhi ameongoza mamilioni ya Wairani katika zoezi la
upigaji kura ambapo amepiga kura yake na kuwataka wananchi waliotimiza
masharti ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi kutekeleza haki yao ya
kidemokrasia. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema punde
baada ya kupiga kura kwamba, maadui wa Iran wamejaribu kutumia kila njia
kuwashawishi wananchi kutoshiriki uchaguzi wa rais lakini njama zao
zimefeli na zitazidi kufeli kwani idadi iliyoshuhudiwa hadi sasa katika
vituo vya kupigia kura ni kubwa mno.
Ayatullah Khamenei amesema matokeo
ya mwisho yatadhihirisha wazi mapenzi ya Wairani kwa nchi yao na imani
walionayo kwa mfumo. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa mbili
asubuhi na hadi sasa foleni ndefu za wapiga kura zinaendelea kuonekana
katika maelfu ya vituo hapa Tehran na nchi nzima kwa ujumla. Duru ya 11
ya uchaguzi wa rais imewavutia wagombeaji 6 ambao ni; mwakilishi mkuu wa
Iran katika mazungumzo ya nyuklia Saeed Jalili, kamanda wa zamani wa
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mohsen Rezai, mwakilishi wa
zamani wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia Sheikh Hassan Rohani, waziri
wa zamani wa Mawasiliano Mohammad Gharazi, meya wa Tehran Mohammad
Baqer Qalibaf na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Ali Akbar Velayati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment