Afrika Kusini imeafikiana na Libya kurejesha zaidi ya dola
bilioni moja zilizokuwa zimefichwa katika nchi hiyo na dikteta Muammar
Gaddafi. Pravin Gordhan Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini amesema, uamuzi
huo wa kurejeshewa Libya fedha hizo na mali zilizokuwa za Gaddafi
umechukuliwa kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa. Juni 2 magazeti
ya Libya yaliandika kuwa, serikali ya Afrika Kusini ilitakiwa kuisaidia
kuirejeshea serikali ya Tripoli fedha, dhahabu na almasi za Gaddafi.
Imeelezwa kuwa, baada ya uchunguzi kufanywa ilijulikana juu ya Mali hizo
zilizokuwa zimefichwa huko Afrika Kusini na katika nchi nyingine jirani
na Gaddafi pamoja na mkuu wa zamani wa vyombo vya ujasusi vya Libya
Abdullah al-Senussi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, wananchi wa Libya walianza harakati za
kimapinduzi dhidi ya utawala wa karibu miongo minne wa Kanali Muamari
Gaddafi Februari 2011 na kufanikiwa kuuangusha utawala huo Agosti 2011
ambapo Gaddafi aliuawa Oktoba 20 mwaka huo.
No comments:
Post a Comment