Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema kuwa nchi yake itakuwa ya
kwanza kumkaribisha rais mteule wa Iran kwenye makutano wa kimataifa wa
Geneva 2 wa kujadili mgogoro wa Syria. Hollande amenukuliwa na vyombo
vya habari akisema, Sheikh Hassan Rohani aliyechaguliwa kwenye uchaguzi
wa rais uliofanyika Ijumaa iliyopita hapa nchini ni mwanadiplomasia
mtajika na kwamba anaweza kuleta mitazamo yenye kukubalika kwennye
mkutano huo.
Mgogoro wa Syria umetawala vikao vya wakuu wa nchi tajiri
zaidi duniani huku Russia ikisisitiza kwamba mgogoro huo utafutiwe
ufumbuzi wa kisiasa. Hata hivyo Marekani ambayo pia ilishiriki mkutano
huo wa G8 huko Ireland Kaskazini bado inasisitiza kwamba itawapa misaada
ya silaha magaidi wanaopigana kuipindua serikali ya Rais Bashar Asad.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment