Mkutano wa tatu wa wabunge wa nchi za Maziwa Makuu unaendelea huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Katika kikao hicho, washiriki kutoka nchi 12 za Maziwa Makuu
wanajadili njia za kurejesha amani ya kudumu kwenye maeneo yenye
migogoro ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, mashariki mwa DRC, na baina
ya Sudan na Sudan Kusini.
Kikao hicho kilichoanza Jumanne kinatazamiwa kumalizika leo
Alkhamisi. Katibu mtendaji wa mkutano wa kimataifa kwa nchi za Maziwa
Makuu, Ntumba Luaba ametoa wito kwa washiriki kuhakikisha kuwa
wanajitahidi kupitisha maazimio ambayo yatahakikisha makundi
yanayovuruga amani katika eneo la Maziwa Makuu yanatokomezwa ifikapo
mwaka 2014. Amesema kushughulikiwa masuala ya usalama ni jambo ambalo
litatoa fursa kwa harakati za kutokomeza umaskini.
No comments:
Post a Comment