WAKILI wa Kujitegemea Ademba Gomba aliwaumbua waendesha mashtaka
wawili wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuiomba
Mahakama isiwatambue uwakilishi wao, hadi wakavae vizuri.
Omary The Great ilishuhudia mawakili hao wa kike,
Hellen Osujaki na Faraja Sambala wakitinga Mahakamani wakiwa wamevaa
nusu uchi hususan sehemu za vifuani zikionekana hata jinsi cheni zao
zilivyokuwa zimekaa ilikuwa ni aibu tumu.
Kabla ya kesi kuanza watu waliokuwa katika Mahakama hiyo ya Hakimu
Mkazi Kisutu wakiwemo washtakiwa walishindwa kuvumilia aibu hiyo kiasi
cha kuguna na kusema "Duh aibu gani hii".
Kitendo hicho kilimfanya Wakili Ademba aiombe Mahakama isitambue
uwepo wa uwakilishi wa mawakili hao wa Takukuru Mahakamani hadi hapo
watakaporekebisha mavazi yao kwa kuvihifadhi vifua vyao.
Baada ya kutolewa kwa ombi hilo, Hakimu Victoria Nongwa aliyekuwa
amepangiwa kuisikiliza kesi hiyo, aliisimamisha kesi kwa muda wa dakika
10 ili kuwapa nafasi mawakili hao wa Takukuru kuvaa vizuri nguo zao.
Hivyo watu wote pamoja na washtakiwa walitoka nje na ulipomalizika
muda huo, mawakili hao walirudi wakiwa wamevaria nadhifu na mahakama
ikaendelea.
Katika kesi hiyo, vigogo watatu wa Halmashauri ya jiji la Dar es
Salaam walipandishwa kwenye mahakama hiyo, wakikabiliwa na mashtaka ya
kula njama, wizi na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Vigogo hao wanadaiwa kujipatia fedha hizo kutokana na kukusanya mapato katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo ,Washtakiwa hao ni Mhasibu Msaidizi na Afisa Maalipo Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Wengine ni Elida Mponda, Mhasibu na Mkusanya wa Mapato wa
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Geofrey Kibasa na Afisa wa Mapato
wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salam, Ernest Maduhu .
No comments:
Post a Comment