Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani
(ILO) inaonesha kuwa, idadi ya watu wasio na ajira inatarajiwa
kuongezeka mwaka huu na kufikia milioni 202. Ripoti ya kila mwaka ya
Shirika la Kazi Duniani iliyotolewa leo imebainisha kuwa, ikiwa imepita
miaka mitano tangu kuibuka mgogoro wa fedha duniani, idadi ya watu wasio
na ajira inazidi kuongezeka na kwamba, walimwengu wataraji kuona idadi
hiyo ikifikia milioni 202 katika mwaka huu wa 2013.
Aidha ripoti hiyo imezungumzia mwenendo
wa ajira duniani na kubainisha kwamba, mwaka jana takribani watu milioni
nne waliongezeka katika idadi ya watu wasio na kazi ulimwenguni na
kuifanya idadi hiyo kufikia watu milioni 197. Ripoti ya Shirika la Kazi
Duniani inaeleza kuwa, mgogoro wa kiuchumi na matatizo ya fedha
yaliyotokea barani Ulaya ndilo chimbuko kuu la kuongezeka kwa kasi idadi
ya watu wasio na kazi duniani; kwani kabla ya mgogoro huo idadi ya watu
wasio na kazi duniani ilikuwa milioni 28 tu.
No comments:
Post a Comment