Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa,
utawala wa Kizayuni wa Israel ndio unaobeba dhima ya roho za wafungwa na
mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala huo
katili. Taarifa ya Hamas sambamba na kutoa mkono wa pole kutokana na
kuuawa shahidi Ashraf Abu Dhari' mateka wa Kipalestina aliyekuwa
akishikiliwa katika moja ya magereza ya utawala huo ghasibu imesisitiza
kwamba, askari magereza wa utawala huo wamekuwa wakiwatesa mateka na
wafungwa wa Kipalestina kwa adhabu na mateso mbalimbali ya kiroho na
kimwili.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani
vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa Wapalestina katika magereza ya Israel
na kuitaka jamii ya kimataifa pamoja na asasi za kutetea haki za
bninadamu ulimwenguni zichukue hatua za maana ili Wapalestina hao
waachiliwe huru. Aidha Hamas imetoa wito kwa asasi za kimataifa ukiwemo
Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo ziushinikize utawala
wa Kizayuni wa Israel ili uache kuwafanyia unyama wafungwa na mateka wa
Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment