skip to main |
skip to sidebar
Umoja wa Afrika wasema uko tayari kutuma vikosi vya kusimamia amani Congo DRC
Umoja wa Afrika AU umesema kuwa, uko tayari kutuma kikosi cha kusimamia amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayoshuhudia mapigano mashariki mwa nchi hiyo. Hayo yameelezwa na Jean Ping Mkuu wa Kamisheni ya Usalama na Amani wa Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake na kuongeza kuwa, kwa sasa AU inajiandaa kukusanya kikosi cha nchi za eneo kwa ajili ya kwenda kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa Congo. Kikao cha wakuu wa Umoja wa Afrika kinachomalizika leo huko Addis Ababa Ethiopia pamoja na mambo mengine kimetawaliwa na mgogoro wa Mali, mvutano wa Sudan na Sudan Kusini na mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati huo huo, idadi ya raia wanaokimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazidi kuongezeka kila siku.
No comments:
Post a Comment