Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 16, 2012

Afrika Kusini yasisitiza juu ya kuunga mkono kuasisiwa nchi huru ya Palestina

Serikali ya Afrika Kusini imesisitiza tena himaya na uungaji mkono wake kwa suala la kuasisiwa nchi huru ya Palestina. Ibrahim Ibrahim, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesema bayana kwamba, nchi yake inaunga mkono kwa dhati juhudi za kimataifa zenye lengo la kutaka kuasisiwa nchi huru ya Palestina.
Amesema, msimamo wa Afrika Kusini kuhusiana na kadhia ya Palestina unatokana na msingi wa tajiriba ya kihistoria ya nchi hiyo ambayo huko nyuma imewahi kuonja chungu ya dhulma na ubaguzi. Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini ameongeza kuwa, tangu mwaka 1995, nchi yake imekuwa ikiitambua rasmi serikali ya Palestina na kwamba, ingali iko bega kwa bega na jamii ya kimataifa kuhakikisha Wapalestina wanapata haki zao za kimsingi likiwemo la kuwa na nchi yao huru. Amesema, Afrika Kusini inapinga vikali kuzingirwa Gaza, hatua ambayo imezuia kufikishiwa wananchi hao huduma muhimu.

No comments: