Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 16, 2012

Umoja wa Afrika waeleza matumaini yake ya kuundwa serikali mpya ya Somalia hivi karibuni

Umoja wa Afrika umesema kuwa, una matumaini ya kuundwa hivi karibuni serikali mpya nchini Somalia. Hayo yameelezwa na Jerry Rawlings Rais wa zamani wa Ghana na mpatanishi wa wa Umoja wa Afrika na kusema kuwa, umoja huo una matumaini kwamba, hadi kufikia Agosti mwezi ujao uchaguzi wa Bunge utakuwa umefanyika nchini Somalia na kuundwa serikali mpya. Akizungumza pambizoni mwa mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Rawlings amesema, umoja huo unafanya kila uwezalo kuhakikisha kwamba, amani na uthabiti vinarejea nchini Somalia.
Kwa upande wake Ramtane Lamamra Mkuu wa Kamisheni ya Usalama na Amani ya Umoja wa Afrika amesema, umoja huo unapanga kuchukua hatua zaidi za kurejesha amani na uthabiti huko Somalia. Hayo yanajiri kali hali ambayo, hali ya kibinaadamu nchini Somalia inaripotiwa kuwa mbaya hasa kutokana na upungufu mkubwa wa chakula unaoikabili nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

No comments: