Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 16, 2012

Iran yaonya kuhusiana na njama za maadui za kupotosha wimbi la mwamko wa Kiislamu

Kiislamu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuhusiana na njama za maadui za kutaka kupotosha mwenendo wa mwamko wa Kiislamu. Dakta Ali Akbar Salehi amebainisha kwamba, maadui wanafanya njama za kupotosha malengo ya wimbi la mwamko wa Kiislamu katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. Akizungumza hapa mjini Tehran na jopo la maulama wa Kiislamu wa Lebanon, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza kwamba, mwenendo wa mwamko wa Kiislamu umekuwa uko dhidi ya maslahi haramu ya maadui na ndio maana maadui hao wanakesha usiku kucha wakitafakari namna ya kupotosha wimbi hili la mwamko wa Kiislamu. Salehi ameashiria nafasi muhimu ya maulama katika kukabiliana na fitna za maadui katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kwamba, kuweko fikra ya pamoja baina ya maulama ni jambo lenye nafasi muhimu katika kusambaratisha njama za maadui.

No comments: