Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kufuatia kushadidi zaidi mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zaidi ya watu 200, 000 wamelazimika kuhama makwao.
Mapingano hayo ni baina ya vikosi vya serikali na waasi wajulikanao kama M23 ambao wameteka miji kadhaa ya eneo hilo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA limetoa taarifa na kusema wengi wa watu waliohama makwao wamesalia nchini Kongo kama wakimbizi wa ndani, lakini idadi kubwa ya watu wamevuka mpaka na kukimbilia nchini Uganda.
Kwa mujibu wa msemaji wa OCHA, Jens Laerke wafanyakazi wa huduma za kibinadamu wanapata ugumu kuwafikia watu walolazimika kuhama makwao kwa sababu ya usalama. Ametoa wito kwa wahusika katika mzozo huo kutowalenga wanaotoa huduma za kibinadamu kwa waloathiriwa. Amesema ni muhimu wakimbizi kupata msaada wa kibinadamu haraka iwezekanavyo. Nayo serikali ya Uganda imetoa wito kusaidiwa kukabiliana na hali hiyo, na hazina ya fedha za dharura ya Umoja wa Mataifa imetoa pesa ili kusaidia juhudi za kibinadamu katika eneo lililoathiriwa na mzozo huo.

No comments:
Post a Comment