Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 17, 2012

Sudan yaituhumu Malawi kuwa haijaheshimu maamuzi ya AU

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imeishutumu serikali ya Malawi kwa kutoheshimu maamuzi ya Umoja wa Afrika AU. Mtandao wa habari wa Sudan Sifari hii leo umemnukuu Waziri wa Nchi katika Wizara ya mambo ya Nje ya nchi hiyo Salah Wensi akisema kuwa, kitendo cha Malawi kukataa kuwa mwenyeji wa kikao cha Umoja wa Afrika AU kinamaanisha kuwa nchi hiyo inapingana na maamuzi yote ya umoja huo. Wensi amesema kuwa, Malawi ilipaswa iwaalike wajumbe wote wa AU na si kubagua, hata hivyo Lilongwe ilipuuza suala hilo huku ikienda mbali zaidi na kutoa vitisho vya kutaka kumtia mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan. Ameongeza kwa kusema kuwa, tayari Umoja wa Afrika uliwataka wanachama wake kutoitikia mwito wa mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC, lakini Malawi haikutii amri hiyo jambo ambalo linaonyesha kuwa Lilongwe inafuata kibubusa mahakama hiyo na kuizibia masikio kauli ya Umoja wa Afrika.

No comments: