
Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu amewapa amri wajumbe wa baraza lake la mawaziri kufanya haraka iwezekanavyo kuwaondoa wahajiri hao wenye asili ya Kiafrika huko Palestina. Hii ni katika hali ambayo, makundi ya Wazayuni wenye kufurutu ada mapema hii leo wamevamia eneo la mji wa Yafa uliopo katika huko Quds Tukufu na kuchoma moto nyumba moja pamoja na kumjeruhi mtu mwenye uraia wa Eritrea. Vitendo vya ubaguzi vimeongezeka sana hivi karibuni huko Israel kuwalenga wahajiri wa Kiafrika huku serikali ya utawala huo ghasibu ikiwa imekaa kimya.
No comments:
Post a Comment