
Mwezi Mei uliopita utawala haramu wa Israel ulitiliana saini makubaliano maalumu na viongozi wa maelfu ya mateka wa Palestina ambao tokea mwezi Februari walianza kususia chakula, na kuahidi kwamba ungeshughulikia malalamiko yao baada ya wao kuamua kusitisha mgomo wa chakula. Licha ya makubaliano hayo lakini utawala huo ungali unawatia nguvuni mateka na kuwakandamiza.
Kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na hasa mateka wao kumechukua mkondo mpya na hatari katika siku za hivi karibuni. Zaidi ya mateka 5000 wa Kipalestina wanaendelea kuteseka katika jela za utawala huo na hii ni katika hali ambayo mateka wapya wamekuwa wakikamatwa na kurundikwa kwenye jela hizo za kuogofya.
Wafungwa wa Kipalestina zaidi ya 200 wamepoteza maisha yao na mamia ya wenginekukumbwa na magonjwa sugu yasiyotibika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mateso makali wanayopata katika jela hizo. Kuendelea kwa jinai na kukanyagwa kwa haki za kimsingi za Wapalestina ni jambo linaloendelea kuhatarisha maisha yao kila siku.
Katika hali hiyo kimya cha jamii ya kimataifa kimeupelekea utawala huo wa Kizayuni kumea pembe na kuendelea kutenda jinai dhidi ya taifa la Palestina bila ya kujali lolote. Inasikitisha kuona kwamba kila mara mashinikizo ya kimataifa yanapoongezeka dhidi ya jinai za utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia wa Palestina, taasisi za kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa hutoa ahadi hewa za kufuatilia jambo hilo na kisha kutofanya lolote muhimu baada ya kupungua mashinikizo hayo. Fikra za waliowengi duniani zinataka kutatuliwa haraka na tena kwa uadilifu suala la Palestina na kwa hivyo taasisi na mashirika husika ya kimataifa yanapasa kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment