
Habari kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya zinasema kuwa watu wenye silaha wameuzingira uwanja wa ndege wa kimataifa mjini humo na hivyo kulazimu ndege kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa kijeshi viungani mwa mji mkuu huo. Watu hao wanadaiwa kutoka katika mji wa Tarhouna ulioko kilomita 80 kusini mashariki mwa Tripoli. Habari zaidi zinasema kuwa kundi hilo ambalo linaaminika kuwa sehemu ya wafanyamapinduzi waliompindua Muamar Gaddafi linataka kuachiliwa mmoja wa makamanda wake aliyetoweka siku mbili zilizopita na anayedaiwa kuzuiliwa mjini Tripoli. Maafisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Tripoli wamesema hali ni ya wasiwasi kwani kundi hili limejizatiti kwa silaha nzito pamoja na vifaru vya kijeshi na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia katika angatua hiyo.
No comments:
Post a Comment