Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 17, 2012

Sudan Kusini yaendelea kuwaunga mkono waasi katika jimbo la Darfur, Sudan

Mateka walioachiliwa huru na kundi la waasi la Uhuru na Usawa katika jimbo la Darfur Sudan wamesema kuwa, Sudan Kusini inayasaidia makundi ya waasi wanaoendesha harakati za uasi katika jimbo hilo dhidi ya serikali ya Khartoum. Mateka hao wanne walioachiliwa huru wamesema kuwa, huku wakipewa ulinzi na wanajeshi wa Sudan Kusini wapiganaji wa kundi hilo la Uadilifu na Usawa hivi karibuni walilishambulia eneo la Fataha katika jimbo hilo la Darfur.

 Mmoja wa viongozi wa jimbo hilo la Darfur Ahmad Sinin amethibitisha habari ya mateka hao na kuongeza kuwa, Sudan Kusini ni muungaji mkono nambari moja wa makundi ya waasi katika jimbo hilo. Itakumbukwa kuwa, mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Sudan na waasi katika jimbo la Darfur yalianza mwaka 2003 ambapo mamia ya maelfu ya watu waliuawa. Nao wachambuzi wa mambo wameonya kuhusiana na njama za kujitenga kwa jimbo hilo na kuongeza kuwa, mchezo wa Sudan Kusini hautakiwi ujirejee tena nchini humo.

No comments: