
Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina na ambaye aliongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marc Ravalomanana, hivi karibuni anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na hasimu wake huyo. Andry Rajoelina ameyasema hayo hapo jana alipokuwa akizungumza na mpatanishi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC na kuongeza kuwa, amekubali kufanya kikao cha pamoja na aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Marc Ravalomanana ili kumaliza mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Mwanzoni mwa mwezi huu nchi 15 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Ustawi wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC ziliazimia kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Madagascar sambamba na kuwashawishi mahasimu hao kukaa katika meza moja ya mazungumzo na kumaliza suitafahamu baina yao. Aidha SADC imesema kuwa, mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 26 ya mwezi huu baada ya kumalizika sherehe za uhuru wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment