Muncef al Marzouki, Rais wa mpito wa Tunisia
Rais Moncef al Marzouki wa Tunisia amesisitizia haja ya kuimarishwa zaidi uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ametoa mwito huo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na televisheni ya al Alam na kuongeza kuwa, uhusiano wa nchi hizi mbili za Kiislamu ni mzuri kwani taifa la Tunisia halina hitilafu zozote za kimsingi na ndugu zao wa Iran.
Amesema nchi yake inakaribisha juhudi zozote za kustawishwa uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala yote.
Rais huyo wa mpito wa Tunisia pia amesema, Tunis inaunga mkono haki ya Iran ya kutumia nishati ya nyuklia katika masuala ya amani na wakati huo huo inapinga nchi yoyote ile duniani kumiliki silaha hatari za nyuklia.

No comments:
Post a Comment