
Mlipuko huo umetokea leo mchana karibu na ofisi za iadara ya Waqfu wa Mashia katika eneo la Babul Muadham lililoko mjini Baghdad na kuwaua watu 32 sambamba na kuwajeruhi wengine wapatao 100. Katika tukio hilo la kigaidi nyumba kadhaa za idara hiyo pia zimeharibiwa huku wafanyakazi wengi wa idara hiyo wakiwemo polisi wa usalama wakiuawa. Kufuatia tukio hilo vikosi vya usalama vya mjini Baghdad vimezingira eneo la tukio hilo na kuanzisha uchunguzi ili kuwatia nguvuni waliohusika na tukio hilo la kigaidi.
No comments:
Post a Comment