
Mapigano hayo yametokea baada ya kuuliwa kijana mmoja katika kituo kimoja cha polisi magharibi mwa mji huo.
Duru za kuaminika zinasema kuwa, mapigano hayo yaliendelea hadi katikati ya jana usiku kwenye kituo cha polisi wa jeshi mjini Bengazi.
Huku hayo yakiripotiwa, watu wenye silaha jana walidhibiti kwa muda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mjini Tripoli na kulazimisha ndege zilizokuwa zinaingia mjini humo kutua kwenye uwanja mmoja wa kijeshi.
Habari hizo zinasema kuwa jana kundi moja la wanamgambo liliuvamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tripoli wakiwa na vifaru na magari ya kijeshi na kuzuia kikamilifu eneo la kutua na kurukia ndege.
Wanamgambo hao walikuwa wanataka kujua hatima ya kiongozi wao Oegeila al Hebeishi aliyekuwa ametiwa mbaroni mapema jana.
Vyombo vya habari vya Libya vimetangaza kuwa wanamgambo hao waliondoka uwanjani hapo baada ya kuhakikishiwa kufanyika uchunguzi kuhusu kutiwa mbaroni kiongozi wao huyo.
No comments:
Post a Comment